Kipengele cha premium kwenye Boomplay app, ni kipengele kinachokuwezesha mtumiaji kujiunga na subscription plan zetu mbalimbali zinazopatikana katika app. Katika kipengele hiki ndipo unapeweza kuona aina zote za subscription tulizonazo na gharama zake.


Unaposubscribe kwenye plan yetu yoyote, unakuwa mwanachama wa Boomplay wa VIP na hii hukuruhusu kusikiliza nyimbo bila matangazo na kupakua nyimbo na video zisizo na kikomo kucheza ukiwa offline. Ili kupakua nyimbo unahitaji data, lakini, kusikiliza hauitaji data.


Fungua app kisha bofya alama ya Premium


Ukurasa wa Premium utafunguka, utaweza kuchagua plan unayopenda kujiunga nayo, kisha utabofya Subscribe Now.


Pia unaweza kuona playlist, points na zawadi zinazopatikana ukijiunga na kifurushi cha Premium