Nyimbo zilizopakuliwa kupitia subscription haziwezi kuhamishwa kutoka simu ya zamani kwenda kwenye simu mpya. Miziki yote inayopakuliawa sasa inakua katika mfumo wa bp. Na unaweza kusikiliza ndani ya app tu.  

Lakini, unaweza kuhifadhi (Backup) nakala za nyimbo zako kwa kuhamisha faili kwenye memori kadi   kutoka simu ya zamani kabla ya kubadili kwenye simu mpya. Pia Favorites na Playlist zako zitaendelea kupatikana katika simu yako mpya.


Fata hatua zifuatazo kuhamisha mafaili yako kutoka simu ya zamani kwenda kwenye memori cadi.


Hatua ya Kwanza: Nenda kwenye file manager katika simu yako, fungua memori kadi, na kasha tengeneza folder kisha uliandike ‘Boom Player’ na fungua folder original la 'Boom Player'.


Hatua ya Pili: Fungua internal storage (phone memory) Chagua folder la ‘Download’, na kisha utachagua CUT (tafadhali usili copy)


Hatua ya Tatu: Rudi katika memori kadi yako na kisha PASTE ndani ya folder la ‘Boom Player' ambalo ulilitengeneza  jipya.


Hatua ya Nne a: Nenda tena  kwenye file manager na ufungue memori kadi  tena.


Hatua ya Nne b: Fungua folder lako jipya la Boom Player na kisha bofya  katika Downloads kuangalia nyimbo kisha unaweza kutoka kwenye file manager.


Hatua ya Tano: Fungua app kwenye simu yako, na kisha log out. Ukiwa bado umelog out, nenda kwenye downloads, na kisha hautaoni kitu chochote humo.


Hatua ya Sita: Log in tena kwenye app, nenda kwenye downloads,   na utaona  nyimbo zote ulizopakua (downloads)


Kumbuka:

1. Tafadhali kumbuka ku CUT na sio ku COPY wakati unahamisha mafolder.

2. Mafaili yanatakiwa kubaki kwenye memori kadi yako ili uweze kuplay nyimbo hizo.