1. Boomplay ni nini?

 

Boomplay ni app ya muziki inayotoa huduma ya kusikiliza na kupakua nyimbo, pamoja video, na  habari kede kede za burudani.

 

 

2. Napataje application hii?

 

App ya Boomplay App inapatikana kwenye simu za Android na iOS.

 

Kama unatumia simu ya Androi, unaweza kupakua app hii kutoka Google Play Store and na kama unatumia simu ya iOS, unaweza kupakua app hii kutoka App Store.

 

Boomplay pia inapatikana katika simu za Infinix, TECNO & itel phones.

 

 

3. App ya Boomplay inafanyaje kazi?


 

App ya Boomplay Music inakuwezesha kupata nyimbo zaidi ya milioni, video za kutosha na habari kede kede za burudani. 

 

Unaweza pia kutengeneza playilist ya nyimbo upendazo, ukashea pia na marafiki na watumiaji wengine.

  


4. Ni huduma zipi zinapatikana ndani ya app?

 

Huduma zipatikanzao ni pamoja na; 


•    Kusikiliza nyimbo na video

•    Upakuaji wa nyimbo na video

•    Utengenezaji wa Playlist

•    Habari za burudani na michezo

•    Crossfade

•    Equalizer

•    QR Scanner

•    Kucomment, kufollow, na kuchat

•    Sleep Timer

•    Web player service


Na mengi zaidi….

 

 

5. Jinsi ya kupakua app.


Kama wewe ni mtumiaji wa Android, basi fata hatua zifuatazo kupakua app ya Boomplay.


1. Fungua Play store, na kisha tafuta app ya Boomplay 2. Kisha bofya kipengele cha Pakua (Install)
3. Utakua umepakua app hii na unaweza kufungua tayari kutumia.
Kama wewe ni mtumiaji wa iOS, basi fata hatua zifuatazo kupakua app ya Boomplay.


1. Ingia katia App Store, kisha tafuta Boomplay 2. Kisha Bofya alama ya Kupakua 3.Utakua umepakua app yako na tayari unaweza anza kuitumia