Kuna Njia mbili za kupakua nyimbo kwenye app: Kupakua kwa njia ya Kusubscribe na kupakua bure/free.


Angalia njia zote mbili kama ifuatavyo.


1. Kupakua nyimbo kwa njia ya Subscription (VIP)


Hapa utaitaji kusubscribe kwanza kabla ili uweze kupakua nyimbo nyingi uwezavo, na utaweza kuplay nyimbo hizi ukiwa offiline, yani kucheza nyimbo bila internet. 


Kumbumbuka: Nyimbo zilizopakuliwa kupitia subscription haziwezi kuchezwa nje ya app, yani kwenye media player nyingine. Pia nyimbo hizi zitapatikana tu pale subscription ikiwa haijaisha. Ikiisha itakubidi kurenew tena ili kusikiliza nyimbo offline. 


Chagua wimbo/album upendayo na kisha fata hatua zifuatazo. Pia tambua kuwa unaweza kupakua album kwa kubofya alama ya Download kisha kufata maelekezo.


1. Bofya kwenye alama ya doti tatu pembeni ya nyimbo au video yoyote. (Unaweza kupakua nyimbo kupitia alama zote nyekundu katika picha hapo chini)


2. Bofya Download


3. Fata maelekezo yatakayofuata na utakua umepakua nyimbo.


Kumbuka: Unaweza kuangalia maendeleo ya nyimbo ulizopakua katika Library chini ya Downloads and Local Music


Kama upakuaji wako umesisima(paused), bonyeza Pause/Resume nyimbo unazopakua na zitaendelea kudownload. Unaweza kutumia njia hii pia kufuta nyimbo. 


Unaweza pia kuangalia historia ya nyimbo ulizopakua katika app kwa kubofya kwenye library, kisha Download & Local Music, kisha gonga kwenye alama ya duara. 


2. Upakuaji wa nyimbo Bure/Free.


Unaweza kupakua nyimbo bure. Nyimbo zinazopakuliwa bure zina alama ya 'Free' pembeni ya alama ya Download.


1. Bofya alama ya vidoti vitatu pembeni ya nyimbo au video yoyote.

2. Bofya Download


3. Kisha fata maelekezo yanayofata na nyimbo zako zitakua zinadownload.



Kumbuka:


1. Nyimbo zilizo na alama ya 'Free' pembeni ya sehemu ya Download option, unaweza kudownload nyimbo hizo bure kabisa bila Boomplay Subscription.


2. Nyimbo zenye alama ya 'VIP' pembeni ya sehemu ya kudownload, haziwezi kupakuliwa bila kuwa na Boomplay Subscription.


3. Unaweza kupakua Album au playlist yote kwa kubofya alama ya download (mshale wa downward) na ukafata maelekezo badala ya kupakua nyimbo moja moja.